Rais wa Tanzania Academy of Science (TAAS) Prof,Esther
Mwaikambo, akizungumza katika Hafla ya
kuwatunuku watafiti wa Sayansi jana
katika ukumbi wa COSTECH uliopo jijini Dar es Salaam.
CHAMA cha wanasayansi Tanzania (TAAS) Kimewatunuku kwa
kuwapa vyeti watafiti 110
wa sayansi kutoka katika sekta mbalimbali nchini Tanzania.
Akizungumza katika tukio hilo Rais wa Chama hicho
Prof,Esther Mwaikambo amesema kuwa , tukio hilo ni la kuwatia moyo kutokana na
watafiti kuongezeka tofauti na ilivyokuwa mwanazo ambapo walikuwa watafiti 25
tu.
Prof, Mwaikambo amesema kuwa, lengo lao la kutoa Tunuku hiyo
ni ili Taaluma ya Sayansi iweze kujulikana zaidi kuanzia shule za Msingi mpaka
kwenye vyuo vikuu ambapo watafiti hao watakuwa wakitoa Semina mbalimbali kwenye
Shule juu ya Umuhimu wa Sayansi.
Alielezea changamoto inayowakumba kuwa ni, kutokuwepo kwa
kamusi ya Sayansi itakayowawezesha wanasayansi kujua maneno Magumu yaliyopo katika somo la Sayansi hasa katika shule za Msingi na
Sekondari hata vyuo ambapo wanafunzi wanakumbana na Matatizo hayo.
Kutokana na Changamoto hiyo Prof, Mwaikambo amesema
kuwa, Chama kina mpango wa Kutengeneza
kamusi itakayokuwa inatafsiri maneno
magumu ya Kisayansi, ili wanafunzi waweze kuelewa sayansi kwa undani zaidi.
“Kweli tunachangamoto ya Ukosefu wa Dictionary lakini chama
kipo njiani kutengeneza lkamusi ya Kisayansi ambayo tunatarajia ikamilike hivi
karibuni kwani tayari tumesha andika Mradi wa kuomba msaada wa Kamusi hiyo”,
amesema Mwaikambo.
|
No comments:
Post a Comment