RAIS
wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amehahidi
kuwasaidia Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) kwa kuiwezesha kupata
fedha kwa ajili Vitambulisho vya Taifa ili kabla ya uchaguzi wa
mwaka 2015 watu wote watakuwa na vitambulisho vya Taifa vitakavyo tumika
katika uchaguzi huo.
Aidha
Rais Kikwete aliitaka NIDA kutoa vitambulisho kwa watu wanaotakiwa
na kuchukulia hatua za kisheria wale watakaokiuka sheria ya usajili wa
vitambulisho hivyo.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Rais Kikwete wakati uzinduzi wa mfumo wa
usajili na utambuzi wa watu kitaifa na utoaji wa vitambulisho hivyo
uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
Kikwete aliwataka wananchi kuwa wazalendo kwa kutoa taarifa zao kwa
uaminifu na kutoa ushirikiano ili kurahisisha zoezi hilo.
Aliwataka
viongozi wa dini, serikali na waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele
katika kuwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano huo.
Naye
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi alisema ni
muhimu kuwa na vitambulisho vya Taifa kwani ni jambo la msingi ambalo
litaweza kuwa na manufaa makubwa kwa kuunganisha mifumo mikubwa ya
usajili ya kitaifa.
Baadhi
ya mifumo hiyo ni kama Mfumo wa usajili wa kodi(TRA), Mfumo wa vizazi
na vifo(RITA),Mfumo wa pasi za kusafiria(UHAMIAJI),Mfumo wa POLISI,
Mifumo ya mawasiliano ya simu(Vodacom,Tigo,Zantel,Airtel,TTCL),Mfumo wa
Taarifa za kiutumishi na Mishahara Serikalini, Mifumo ya Hifadhi za
kijamii,Mifumo ya Taasisi za kifedha,Mifumo ya udahili ya Wanafunzi(Loan
Board),n.k.
Mkurugezi
Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu alizitaja changamoto mbalimbali za
kiutendaji zikiwemo wananchi kukosa viambatanisho muhimu vya
kuwatambulisha,uhakiki wa taarifa za uraia,Uhakiki wa taarifa za
makazi,Upungufu wa vifaa na Rasilimali watu.
Aliyataja
mahitaji halisi ya zoezi hilo kuwa ni vifaa vya kuchukulia alama za
vidole, picha saini takribani 12,000, rasilimali watu wa muda 114,000
na wakudumu 3000 ili kukukamilisha mpango huo kwa muda utaotakiwa.
No comments:
Post a Comment