Mkurugenzi wa Taasisi ya VEPK Bi, Ketty Allen, akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa
Uzinduzi wa kitabu cha kumwongoza mwalimu kufundisha Kingereza.
|
Serikali imeshauriwa kupitisha Mtaala wa kutumia lugha ya kingereza katika
kufundishia shule za msingi ili kuwasaidia wanafunzi kuielewa lugha hiyo pindi
wanapokwenda katika elimu ya sekondari na elimu za juu.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Taasisi ya Elimu ya mpango wa
elimu vijijini VEPK (village education project Kilimanjaro) Bw Dilly Mtui leo jijini dar es salaam wakati alipokuwa
akizindua kitabu kipya cha mwongozo kwa waalimu wa shule za msingi kitakacho
wasaidia walimu kufundisha kwa ufasaha kiingereza katika shule za msingi.
Bw Mtui amesema
moja ya sababu ya wanafunzi kufeli sana katika elimu ya sekondari ni maandalizi
mabovu wanayoyapata wakati wakiwa shule za msingi,amesema katika shule za
msingi wanafunzi hujifunza kwa Kiswahili jambo linalowawia gumu wakati
wanapoingia sekongari na kukuta masomo kwa lugha ya kiingereza.
Ameongeza kuwa serikali inapaswa kuwasaidia walimu wa shule
za msingi ikiwa ni pamoja na kuwapelekea vitabu vya kutosha na miundo mbinu
mizuri ya kufundishia ili waweze kufikisha elimu bora kwa wanafunzi wao.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bi, Katty Allen MBE amesema kuwa sio tu
wanatoa vitabu kwa ajili ya walimu ila bado wana vitabu vya wanafunzi vya kuanzia Darasa la Kwanza na
kuendelea.
Baadhi ya waaandishi wa habari waliokuwemo katika mkutano huo |
Mratibu wa Taasisi hiyo akifafanua jambo mbele ya waandishi
wa habari
|
Moja ya Kitabu kinachozalishwa na Mradi huo |
No comments:
Post a Comment