Thursday, February 14, 2013

NYOTA WA MBIO ZA WALEMAVU AFRIKA KUSINI AMUUA MPENZIWE KWA RISASI

 Gari za Polisi zikiingia katika hekalu la Oscar Pistorius baada ya taarifa za kifo cha Reeva Steenkamp leo asubuhi. Oscar amemuua mpenzi wake huyo kutokana na wivu wa kimapenzi baada ya mrembo wake 'kuposti' ujumbe uliomkwaza katika mtandao wa Twitter.
Reeva Steenkamp akiwa katika picha ya pamoja na mpenzi wake Oscar Pistorius
Oscar Pistorius akiwa ameshikilia tuzo ya 'Laureus World Sportsperson of the Year' aliyoshinda kutokana na mafanikio yake katika mbio za walemavu.
Mwanamitindo Reeva Steenkamp, 30, akipozi kwa picha wakati wa uhai wake
Oscar Pistorius akishiriki Olimpiki ya Walemavu 'Paralympic' jijini London, Uingereza mwaka jana.
Mwanamitindo Reeva Steenkamp, 30, akipozi kwa picha wakati wa Hafla ya kupokea Tuzo za Sport Industry 2013 hivi karibuni.
Oscar Pistorius akishiriki mbio za Olimpiki ya Walemavu 'Paralympic' zilizofanyika mwaka jana jijini London, Uingereza.
Oscar Pistorius, akiwa katika ngazi za nyumba yake ya kifahari ya Silver Woods Estate jijini Pretoria
Oscar Pistorius akiwa ameshikilia tuzo ya Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde, jijini Glascow, nchini Scotland
Oscar Pistorius kulia akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
 
JO’BURG, Afrika Kusini

Kiini cha kifo cha mwanamitindo Reeva Steenkamp, ni wivu wa mapenzi aliokuwa nao mpenzi wake Oscar Pistorius mkimbiaji wa mbio za walemavu ‘Paralympic’ aliyehisi kusalitiwa kutokana na ‘alichoposti’ marehemu katika mtandao wa Twitter

NYOTA wa kimataifa wa Afrika Kusini wa mbio za walemavu ‘Paralympic’ Oscar Pistorius amekamatwa na polisi baada ya kuripotiwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp, 30.

Reeva alipigwa risasi kichwani na mkononi akiwa nyumbani katika hekalu lao lijulikanalo kama Silver Woods Estate jijini Pretoria, yapata saa 10 alfajiri leo, vyombo vya habari hapa vimeripoti.

Kiini cha kifo cha mwanamitindo Reeva Steenkamp, ni wivu wa mapenzi aliokuwa nao mpenzi wake Oscar Pistorius mkimbiaji wa mbio za walemavu ‘Paralympic’ aliyehisi kusalitiwa kutokana na ‘alichoposti’ marehemu katika mtandao wa Twitter.

No comments:

Post a Comment