Faustine Sungura |
Chama cha NCCR-MAGEUZI Kimetangaza kusikitishwa na kitendo cha taarifa ya katibu wa Bunge kwa
waandishi wa habari juu ya mpango wa kuzuia kurusha matangazo ya bunge moja kwa
moja na badala yake kuyafanyia kwanza uhariri kabla ya kuwafikia walaji.
Hayo yamesemwa na Kaimu katibu mkuu wa chama hicho Bw,
Faustine Sungura wakiti alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika
makao makuu ya Chama hicho yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Sungura amesema kuwa, wanapinga kwa nguvu zote hatua zozote
zinazotaka kuchukuliwa na mamlaka yoyote ya kuzuia matngazo ya moja kwa
moja kutoka Bungeni.
“Tunapinga hatua hizi kwasababu, hoja na au sababu za
kutekeleza azma hiyo kama zilivyotolewa na katibu wa Bunge ni hoja Dhaifu na
Hasi”, amesema Sungura.
Ameendelea kusema kuwa Vurugu zinazotokea Bungeni haziwezi
kukomeshwa kwa kuzuia kurusha Matangazo moja kwa moja bali ni kwa kutumia
Utaratibu na kanuni za Bunge.
Bw, Sungura pia amezungumzia, swala la Ujumbe wa Matusi kwa
Spika wa Bunge na kusema kuwa, kama Anna Semamba Makinda, ni jukumu lake
kuwasiliana na Mwanasheria wake kama atakuwa amedhurika na jambo lolote.
No comments:
Post a Comment