Monday, February 18, 2013

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MWAMINI MALEMI ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA NYUZI ZA MKONGE CHA JESHI LA MAGEREZA, KIHONDA MKOANI MOROGORO.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Malimi Malemi (wa pili kutoka kushoto) akiangalia nyuzi za mkonge ambazo zimeanikwa kwa ajili ya kukaushwa maji kabla ya kuingizwa kiwandani kwa ajili ya kuzilainisha na kuzisafisha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) pamoja na wageni waliotembelea kiwanda hicho wakiangalia mashine ya kubana mkonge kwa ajili ya kupunguza ukubwa kabla ya kusafirishwa.

Msimamizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Nyuzi za Mkonge cha Gereza Kihonda lililopo mkoani Morogoro, Fidelis Muhaya akimuonyesha majani ya mkonge ambayo yamevunwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Malimi Malemi (Kushoto). Katikati ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) pamoja na wageni waliotembelea kiwanda hicho wakiangalia mashine ya kubana mkonge kwa ajili ya kupunguza ukubwa kabla ya kusafirishwa.

Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (katikati) akizishika nyuzi za mkonge zilizokamilika ambazo zipo tayari kwa ajili ya matumizi mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment