POLISI mkoani Mwanza wanamshikilia Imamu wa Msikiti wa Ijumaa, huku
likitangaza kuwasaka masheikh wawili wengine pamoja na Askofu (majina
yote yanahifadhiwa) kwa kuhusika na uchochezi wa kidini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema Imamu huyo wa
msikiti alitiwa mbaroni kwa madai ya kubainika kwamba wanahusika na
usambazaji wa CD za uchochezi ambazo zimekuwa zikihamasisha vurugu
pamoja na mauaji ya kidini ikiwa ni pamoja na suala la kuchinja.
Kwa upande wake Askofu Mpemba wa Kanisa la Tanzania Field Evangelist
yeye anasakwa kutokana na kutoa mkanda wa video (DVD) yenye jina la
‘Inuka Chinja Ule’ wakati mashehe wawili wanasakwa kwa kuhusika na
uandaaji wa mikanda ya video mitatu (DVD) zenye majina ya ‘Unafiki
katika Sensa, Kadhia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na
Uadui wa Makafiri’.
Wakati huohuo, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa
Morogoro, limesema huenda likajitenga na Bakwata Taifa kufuatia hatua ya
Sheikh Mkuu, Mufti Issa Shaaban bin Simba kumvua madaraka Sheikh wa
Mkoa wa Morogoro, Yahya Semwali bila kufuata utaratibu.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment