Thursday, February 28, 2013

MWALIMU MKUU AMCHAPA MWANAFUNZI HADI KUMVUNJA KIUNO

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Loruvani ilioko jijini Arusha,mwalim Cosmas,amempiga mwanafunzi wa darasa la nne viboko visivyoesabika na kusababisha mwanafunzi huyo maumivu makali  ya a kiuno.
 Mtoto huyo ambaye ameumia vibaya sasa amepelekwa kwenye hospitali ya Mount Meru .
 MAASINDA ilipomuhoji mtoto huyo ambaye alikua analia kwa maumivu  na kuongea kwa shida ameeleza kuwa kisa cha yeye kupigwa kiasi kile ni baada ya mwalimu huyo kukagua madaftari ya wanafunzi na kukuta la mtoto huyo limechakaa hivyo kuwaamuru watoto wenzake wamshikie chini ili aweze kumchapa bila usumbufu wowote .


No comments:

Post a Comment