Wednesday, February 27, 2013

LULU:MIMI SIJAOMBA MSAADA!!


LuluLULU ambaye kwa sasa yupo uraiani kwa dhamana huku kesi yake ya tuhuma za kuua bila kukusudia ikiendelea, amesema kuwa hajafungua taasisi yoyote wala kuomba
misaada kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. "Nasikia tu kwa watu eti sijui ninataka wasanii waigizaji kwa ajili ya taasisi yangu, mara nimetoa namba ya simu watu wanichangie ili nitengeneze filamu, sijafanya kitu kama hicho na wala siwezi nahitaji kutulia na kuangalia mambo yangu,"alisema.
Hivi karibuni kupitia facebook kumeonekana akaunti inayotumia picha na majina ya Lulu kwa kuwaomba wadau wa filamu wamchangie fedha kwa njia ya m-pesa na tigo-pesa.
Lulu anatuhumiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa msanii wa filamu, Steven Kanumba, kilichotokea mwaka jana.

No comments:

Post a Comment