Wednesday, February 27, 2013

LADY JAYDEE ft.Prof.JAY-JOTO,HASIRA.

 Lady Jaydee
Mashairi haya yametangulia kabla ya ngoma hiyo inayofahamika kama JOTO, HASIRA ikiwa yameachiwa na Jaydee mwenyewe ili fans waweze kui-catch up ngoma yenyewe itakapotoka.

Chorus:

Hili joto hasira, ambaa
Upepo hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa.
Foleni njia nzima, ambaa
Na pesa hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa

VERSE 1:

Kila siku
nimenuna
Kwanini tunagombana
Tena tunakosoana, kama tumechanganyikiwa...

Na sioni hata maana
Ya si kuzinguana
Yaani kila mtu anajua sana
Au yote sababu ya?, sababu ya?

Rudia Chorus:


VERSE 2:

Mazao twalima wote
Sahani wavuta kwako
Kama chakula tule wote
Kwanini chote kije kwako
Kisu mpini umeshika wewe
Vitisho kunikata mimi mmmmhh
Au yote sababu ya? Sababu ya?

Chorus:

Hili joto hasira, ambaa
Upepo hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa.
Foleni njia nzima, ambaa
Na pesa hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa

Hook:

Uuuuh, sahau sahau shida
Oooh ishi ka ziliisha jana
Say goodbye joto, Rest in Peace Shida
Knock, knock money

RAP:

Wenyewe wanasema usawa unakaba
Na rafiki wa kweli ni mama na baba
Hawa wengine wala usiwaamini
Maana binadamu wa sasa wana roho saba
Watakuwa na wewe kwenye raha
Na hawatakuwa na wewe kwenye njaa
Bora nipige misele yangu peke yangu
Niruke kivyangu na woga niliukataa
Aaah!! Nabadilika kama saa
Na Siku hazigandi na sitokataa tamaa
Wamejaa, usaliti na chuki
Watu wa karibu wanageuka mamluki
Jenero nasonga iwe joto au baridi naamini tutashinda
Kama mbwai iwe mbwai barida
We make more money rest in peace shida
Ukinuna unataka tunune wote
Ukilia unataka tulie wote
Vita vyako tunapigana wote
Tukishinda tushinde au bora tufe wote
Kama kulima kote tumelima wote
Hata kupanda kote tumepanda wote
Kupalilia tumepalilia wote
Aaaargggh !!! nashangaa sasa mbona hatuvuni wote??

Chorus:

Hili joto hasira, ambaa
Upepo hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa.
Foleni njia nzima, ambaa
Na pesa hakuna

Ambaa, naruka mwenyewe

Yelela, yelela, ambaa
MWISHO

No comments:

Post a Comment