Friday, January 4, 2013

STAR TIMES WAWASHAURI WATEJA WAO KUELEKEZA ANTENA UPANDE WA KISARAWE ILI KUEPUKANA NA TATIZO LA KUGANDA KWA PICHA

Wakati tukisubiria Muhusika wa kuja kuongea na Sisi ambaye ni Meneja Mauzo wa Star Times Waandishi tulikaribiswa na Soda mojamoja  tukaanza kujiburudisha.

Hatimaye baada ya Robo saa aliwasili Muhusika Mwenyewe ambaye ni David Kisaka Meneja Mauzo wa Star Times pichani akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa, Wateja wa Vin'gamuzi vya Star Times wataanza kufaidika zaidi na Vin'gamuzi vyao baada ya Mtambo mwingine kumalizika kujengwe katika maeneo ya Makongo juu jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa utamalizika baada ya miezi mkiwili.
 Ameongeza kuwa baada ya Mtambo huo kumalizika wateja wa Dar es Salaam hawatapata shida tena ya tatizo la kuganda kwa Picha ambalo baadhi ya Wateja wanakumbana nalo.

Mpaka sasa Star Times inarusha chaneli 9 za kiswahili na wana mpango wa kuongeza nyingine hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Star Times Bw, William Lan akionyesha Mfano wa Antena ambayo Mteja wa Star Times atatakiwa kutumia ili kuepukana na kuto onekana kwa baadhi ya chaneli katika Vin'gamuzi vyao. Bw, Lan amesema kuwa wateja wengi wanaopata matatizo ya kuganda kwa Picha katika Vin'gamuzi vyao wanatumia Antena zisizo sahihi. Ameongeza kuwa baada ya kuweka Antena hiyo Mteja anatakiwa kuielekezea Upande wa Kisarawe ambapo kuna Mtambo wa Star Times.

Baadhi ya Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini.

No comments:

Post a Comment