Wananchi wa Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kulipa Kodi kwa
Uaminifu kwani pesa hizo zinatumika katika kazi mbalimbali katika jamii ya
Manispaa ya kinondoni.
Hayo yamesemwa leo na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw,
Yusuph Mwenda, wakati alipo fanya Ziara ya Kutembelea Bara bara Mpya
Inayojengwa ya Kwenda Ubungo Makoka Jijini Dar es Salaam ambapo katika Maradi
huo Nyumba Tisa Zimebomolewa ili kupisha Ujenzi wa Barabara hiyo na Nyumba hiyo
Zimelipiwa Fidia ya Shilingi Milioni 187.
Mwenda amesema kuwa, Pesa hizo kiasi cha Shilingi 187
Milioni zimetokana na Wananchi wa waaminifu wanaolipa Kodi na hivyo amewataka
Wananchi waendelee kulipa Kodi.
“Naomba wananchi wa Kinondoni waelewe kabisa namna kodi zao
zinavyotumika, Fidia hizi zimetokana na Wananchi kulipa kodi hivyo nawataka
wananchi wote walipe kodi ili Ziweze kuwasaidia wenyewe”, amesema Mwenda.
Hii ndiyo Barabara Mpya ya Ubungo Makoka aliyoitembelea Meya leo, katika Barabara hii tayari zimebomolewa nyumba Tisa zilizokuwa maeneo haya na kulipiwa Fidia |
Engineer wa Manispaa ya Kinondoni akifafanua jambo juu ya namna Mradi utakapo kwenda Mbele ya Mstahiki Meya |
Tupo Ziarani japo kuna Matope |
No comments:
Post a Comment