Na Ali Issa Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzíbar
imetoa taarifa rasmi ya kuruhusiwa kufanya mitihani ya kidato cha
sita, mwezi Februari mwakani, wanafunzi wote 243 wa Zanzíbar waliopewa
barua za kusimamishwa kufanya mitihani hiyo kwa kukosa sifa za kuwa na
alama tano.
Taarifa hiyo imetolewa leo na
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzíbar, Ali Juma Shamhuna huko
Ofisini kwake Mazizini mjini wakati alipokutana na wandishi wa habari.
Waziri Shamhuna amesema maamuzi
hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo yake na Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi wa Tanzania Bara Dk. Shukuru Kawambwa yaliyofanyika tarehe 30
Mwezi uliopita mjini Dar es salaam.
Ameseama kutokana na maamuzi hayo
wanafunzi wote waliosajiliwa kufanya mitihani watafanya mitihani yao
baada yamarekebisho ya kasora zilizojitokeza ambazo zilisababishwa na
baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Elimu Bara kujichukulia mamlaka
bila kuijulisha serikali ya Zanzíbar.
“Masula ya Elimu ya juu ni
masuala ya Muungano, hivyo maamuzi yake yanapaswa kuwa ya pamaja kwa
kushirikisha vyombo husika ambavyo vipo kwa mujibu wa taratibu na sheria
kuwatumikia wananchi wa pande zote mbili za Tazania.na si vyenginevyo”.
alisema Shamuhuna.
Alisema maamuzi ya awali ya
kuwasimamisha wanafunzi waliokuwa hawana alama tano, yalitolewa bila ya
kuwepo kikao halali cha Baraza la Mitihani Tanzania NECTA na
lililofanyika ni kuwaandikia barua walimu wakuu wa skuli za Zanzibar
jambo ambalo halikupaswa kutekelezwa kwani vipo vyombo vimewekwa
kisheria na taratibu za kufuatwa.
“Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi ya Tanzania Bara mweziwe ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
ya Zanzbar, ilitakiwa Katibu Mkuu Bara amuandikie barua rasmi Katibu
Mkuu wa Zanzibar kumueleza juu ya mabadiliko yaliyofanyika na sio
kuandikiwa walimu wakuu wa skuli juu ya mabadiliko hayo”.alisema
Shamuhuna
Waziri Shamhuna alisema Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inawajumbe wanne katika Baraza la
mitihani la Tanzania ambao wao hawajui kupitishwa kwa maamuzi hayo
ispokuwa walikua wakifuata agizo la Serikali ya Mungano.
Aliwataja wajumbe hao kuwa ni
Kamishina Baraza la mitihani, Mkurugenzi elimu ya juu, Mkurugenzi wa
Taasisi na lugha za kigeni na mjumbe mwengine kutoka Chuo Kikikuu cha
Taifa Zanzíbar (SUZA).
Waziri Shamhuna alisema pamoja na
kasoro hiyo iliyojitokeza bila kutegemewa, Wizara hizo mbili za Elimu
za Tanzania Bara na Zanzíbar kwa muda mrefu zimekuwa zikifanya kazi kwa
mashirikino makubwa na kuleta ufanisi wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment