MKUTANO
Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) utafanyika Desemba 21 na 22 mwaka huu Kiromo View Resort Hotel,
Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkutano huo unatarajiwa
kushirikisha wanachama 100, na pia watakuwepo wadau mbalimbali wa TASWA
wakiwemo waandishi wakongwe wa habari za michezo wambao watapewa nafasi
ya kuzungumza kwenye mkutano huo.
Wanachama wa TASWA watapata fursa
ya kupokea na kujadili Ripoti ya Utendaji ya chama, Mapato na Matumizi,
maendeleo ya chama na masuala mbalimbali yanayohusu waandishi wa habari
za michezo kwa ujumla.
Pia kutakuwa na semina maalum
itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo ili wawe na uelewa
kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo itajadiliwa
kwenye mkutano huo.
Kamati ya Utendaji ya
TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea kwa
kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza
iwaite wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo
hilo na kukishakuwa na uelewa wa kutosha suala hilo lipelekwe kama
ajenda kamili ya kuanzisha chama hicho kwenye Mkutano Mkuu.
Nia yetu ni kuona tunapiga hatua
za kimaendeleo na kuwafanya wanachama wetu wafurahie kujiunga na chama
hiki na waweze kupata mikopo ya kuwasaidia katika masuala mbalimbali.
Tunawaomba wanachama wote ambao
wanatarajia kuhudhuria mkutano huo wathibitishe ushiriki wao kwa Katibu
Mkuu wa TASWA kwa njia ya email: mgosius@yahoo.com au taswatz@yahoo.com.
Mwisho wa kuthibitisha ni Desemba 15, 2012 saa kumi alasiri ili
maandalizi mengine yaendelee na uwepo wao katika mkutano uthaminike.
Wanachama ambao wanajua
hawajalipa ada ni vyema wakafanya hivyo, kwa kuwasiliana na Mhazini
Mkuu wa TASWA, vinginevyo chama kitafanya utaratibu mwingine wa
kuhakikisha ada zao zinapatikana siku ya mkutano.
TASWA inaendelea na mazungumzo na
wadhamini mbalimbali na Jumatatu Desemba 10, 2012 saa tano asubuhi
katika mgahawa wa City Sports Lounge Dar es Salaam itatangaza mdhamini
wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment