Wasanii wanazidi kuwaza kila siku jinsi ya kukwepa kuibiwa
kazi zao ambazo ni jasho lao wanalotoa booth baada ya kusumbua akili zao na
kufanyia kazi vyema mtaji wa kipaji walichopewa na Mungu.
Asilimia 90 ya wasanii wa Hip Hop hawapeleki kazi zao kwa
wasambazaji bali huuza wenyewe ili kukwepa kuwafaidisha watu wengine kwa jasho
lao.
Staili ya uuzaji iliyopewa jina la ‘kuuuza tapes kwenye bag’
inazidi kupatiwa mbadala kama sio kuboreshwa ili kuwafikia watu wengi zaidi.
Roma mkatoliki ambae ametambulisha wimbo wake alioupa jina
la ‘2030’, wimbo ambao unasubiriwa kwa huwa hadi sasa na fans wake kibao waweze
kuupakua kwenye mtandao, sasa amekuja na staili tofauti ambapo anauuza wimbo
huo kwa Tsh. 3000 tu .
Roma kupitia ukurasa wake wa facebook, ameelezea kuwa mteja
wake atatuma pesa hiyo kwa njia ya simu pesa na email yake ama atatumiwa kwa
njia ya Whasapp, kisha Roma atamtumia wimbo huo, lakini kwa makubaliano pia
kuwa hatausambaza wala kuugawa ili kusapoti kazi yake iendane na kipato chake.
Roma anasema kwa wale ambao hawana uwezo wa kununua basi watausikiliza tu
redioni.
Nikki wa pili |
Nikki wa Pili ambae ni msemaji wa WEUSI pia alizindua aina
mpya ya usambazaji wa kazi za wasanii akianza na kazi yake, na hiyo December
23, katika tamasha la ‘Funga Mwaka la Weusi’ lilifanyika Dar-es-Salaam, Club
Maisha, ambapo walizindua rasmi DVD ya Kum Kubam na wimbo mpya wa Lord Eyez “No
More Drama”.
Katika aina hii mpya ya usambazaji, Mteja ama shabiki
anatakiwa kutuma pesa kwa njia ya M-Pesa kiasi cha Tsh. 4,000 kisha atapewa
CODE NUMBER ambayo ataipeleka kwa wakala wa Fichuka Dar na kupewa DVD hiyo ya
BUM KUBAM.
Siku moja baada ya tamasha hilo, WEUSI waliwatumia watanzania ujumbe
ulioandikwa KUM KUBAM kama Attention kisha ukasomeka hivi;
“kupata CODE NUMBER
ili ukachukue BUM KUBAM DVD kwa wakala wa Fichuka Dar, Lipa kwa MPESA,Namba ya
kampuni 212121,Kumbukumbu Na. Malipo BUM KUBAM, kiasi 4,000.”
Kwa kweli sasa wasanii wanaonesha kuwa na muamko wa vitendo
zaidi na kuutumia vizuri ulimwengu wa sayansi na technolojia, nice Move Roma na
WEUSI, mwaka 2013 ukiongeza sapoti wasanii waliyoahidiwa na serikali najua
tutafika mbali.
No comments:
Post a Comment