Hawa ni waanishi wa Habari waliohudhuria kwenye Mkutano baina yao na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova leo katika makao kuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. |
Jeshi la Polisi Tanzania Limeahidi kufanya Doria kipindi
hichi cha Kusherekea Mwaka Mpaya wakati wa Kupokea Mwaka mpya ambapo Doria itaanza kufanyika leo usiku
katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo katika makao makuu ya
jiji la Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda maalum Suleiman Kova amesema
kuwa, Madereva wanatakiwa Kuzingatia
Sheria za Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha vyombo vya Moto kwa
mwendo kasi na pasipo kulewa.
“Jeshi la [olisi litawashughulikia Madereva wote
wanaoendesha Magari kwa Mwendo kasi, na pia wakiendesha vyombo vya moto vyenye
sauti kali zenye kuleta Mshtuko”, amesema Kamanda Kova.
Aidha Kamanda Kova ametoa tahadhari kwa Wananchi kutochoma
Matahiri au vitu vyovyote kama hivyo vinavyoweza kuharibu miundombinu na kusema
kuwa vikosi vya Zima Moto vitahusika.
Polisi wataweka ulinzi kwenye Fukwe za Bahari kwa kuweka
Vituo vya Polisi vinavyohamishika.
Waandishi wapo Makini kumsikiliza Kamada Kova |
Umati wa waandishi wakishuhudia Tukio la Ufunguzi wa Shampein |
No comments:
Post a Comment