OMBAOMBA1
4 watasafirishwa makwao baada ya kukamatwa ndani ya Kituo cha Mabasi
yaendayo mikoani na Nje ya nchi , Ubungo (UBT), wakiishi kama makazi yao
ya kudumu kinyume cha sheria.
Akizungumza na Fullshangweblog jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Kituo hicho Juma Iddi, alisema ombaomba hao walikamatwa wiki moja iliyopita na kufikishwa katika Mahaka ya jiji.
Alisema uwamuzi wa kuwasafirish
watu hao umetokana na hukumu iliyotolewa na Mahaka kutokana na kuwabaini
kuwa walikuwa na makosa, hata hivyo, kutokana na hali zao iliamuru
warudishwe makwao ikiwa ndiyo adhabu yao.
Iddi alisema watu hao
watarudishwa nyumbani kwao kwa kulipiwa nauli na Mamlaka ya jiji, ambapo
watakaporudi tena Malaka hiyo haitawasamehe.
“Mikakati yetu ni kuondoa kero
zote kwa abiria wetu, angali ombaomba hawa baadhi yao ni wakorofi na
wamekuwa wakiishi humu miongoni mwao wakifanya ngono hadharani kwa
makusudi sasa hali kama hii haikubaliki katika jamii”alisema Iddi.
Vilevile alisema operesheni hiyo
ni endelevu na hawatorudi nyuma bali wanawatahadharisha wale wote
wanaoendesha shughuli zao bila ya kufuata sheria watambuwe kuwa wakati
wao wakuchukuliwa hatua za kisheria umefika.
Iddi alibainisha kuwa opersheni
inaenda kwa awamu ambapo ya kwanza imejihusisha na kuwaondoa ombaomba
inayofuata itawahusu wapiga debe, wachafuzi wa mazingira, vibaka na
kundi la watoto ambalo linaonekana kuongezeka katika kituo hicho.
Hata hivyo, operesheni hiyo ili
iweze kuzaa matunda bado ushiriki wa wadau wa kutoa taarifa kwa
wasimamizi wa kituo hicho unahitajika.
No comments:
Post a Comment