Mpambano wa kugombea ubingwa wa
IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati
utafanyika wakati kukiwa na mzozo wa mpaka wa ziwa Nyasa kati mya
Tanzania na Malawi.
Mpambano huo unaowakutanisha
Mtanzania Francis Cheka na Mmalawi Chimwemwe Chiotra unafanyika katika
jiji la Arusha na linategemea kujenga uhusiano kati ya nchi hizi mbili
zenye mahusiano ya muda mrefu.
Bondia
Chimemwe Chiotra ni mwanajeshi kutoka katika jeshi la Malawi na alianza
harakati zake katika ngumi za kulipwa mapema kabisa na kujizolea sifa
kemkem ambazo zimemwezesha kukubaliwa na IBF kugombea mkanda wake.
Chimwemwe
aliingia katika jiji la Arusha kwa mbembwe tarehe 20 akifuatana na
kocha wake Daudi Kikwanje na kudai kuwa wamekuja kuuchukua mkanda huo wa
IBF waupeleka nchini Malawi ambako ndipo unapostahili kukaa.
Naye
Francis Cheka ambaye ni bingwa wa mikanda mingi pamoja na IBF katika
bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ametamba
kumwonyesha mwanajeshi huo wa jeshi la Malawi jinsi ngumi zinavyotakiwa
kuchezwa. Cheka ametamba kuwa ataubakiza mkanda huo hapa Tanzania kwani
ndipo mahala unapostahili kukaa!
Mpambano
kati ya Francis Cheka na Chimwemwe Chiotra wa Malawi umekuwa gumzo
kubwa katika jiji la Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma pamoja
an chi jirani za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.
Wapenzi
wengi kutoka maeneo hayo wanategemea kufurika kwa wingi jijini Arusha
tayari kuushughudia mpambano huo uliopewa jina la “Vurumai chini ya
Mlima Meru” na wakazi wengi wa jiji hilo lililofunguliwa rasmi kuwa jiji
hivi karibuni.
Viongozi
wengi wakiongozwa na Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo watahudhuria
mpambano huo ambao utafungua rasmi jiji la Arusha kuwa Las Vegas ya
ngumi katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati.
IBF
imewateua Onesmo Ngowi kuwa msimamizi mkuu akisaidiwa na Nemes
Kavishe(Refarii), Boiniface Wambura (Jaji), Mark Hatia (Jaji) na Galous
Lingongo kutoka jiji la Tanga kama jaji.
Nayo TPBC imewateua pia waaamuzi hao kusimamia mapambano ya utangulkizi.
No comments:
Post a Comment