Sunday, December 23, 2012

MTATIRO WA CUF ASEMA KUNA VIONGOZI WASOMI WASIOKUWA NA AKILI

Kaimu katibu Mkuu wa CUF Bw, Julius Mtatitiro amesema kuwa hapa Tanzania kuna viongozi wa aina Mbili ambapo amewataja aina ya Viongozi hao kuwa ni Viongozi waliosoma na wale ambao hawajasoma na kuongeza kuwa kuna viongozi waliosoma wenye Akili na Viongozi waliosoma wasio na akili.
Bw, Mtatiro ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa makao makuu ya Ofisi hizo, baada ya kuulizwa swali na muandishi wa Habari kutoka gazeti la Citizen Aloyce mpanda, swali lenyewe lilikuwa hili always wasomi wamekuwa wakisema Vyama vya siasa vinataka katiba mpya kwa ajili ya uchaguzi mkuu lakini sio kwa ajili ya usawa katika jamii jee unalipi la kuzungumzia kuhusiana na hili?

Mtatiro alitoa mfano wa viongozi wasiokuwa na akili pasipo kuwataja majina kuwa ni wale walioficha Pesa zao katika Benk ya Uswis ambapo amesema kuwa viongozi hao hawana akili kwani ikitokea bahati mbaya wamekufa pesa hizo hazita msaidia yeye bali zitaishia Uswis.
"Wasomi wengine hawana akili sasa msomi mzima unaenda kuficha pesa Uswis? je ikitokea siku moja umekufa Ghafla nani atafaidi hizo pesa? si watakuwa wamewafaidisha watu wa USWIS badala yao weo na familia zao?", amesema Mtatiro ndipo akaendelea kujibu swali aliloulizwa.

No comments:

Post a Comment