Sunday, December 23, 2012

CUF NA LAANA ZAKE PAMOJA NA MATAMKO JUU YA MAOVU YANAYOTENDWA NCHINI,

Naibu katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Bw, Julius Mtatiro akizungumza na waandishi wa Habari leo katika makao makuu ya Chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam.



 
Chama cha wananchi CUF kimeendelea kutoa laana kwa vitendo viovu  vinavyotokea hapa nchini kama ilivyo kawaida ya chama hicho kutoa laana kwa vitendo hivyo.
Leo katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo Naibu katibu mkuu wa Chama Bw, Julius Mtatiro, hicho alikuwa akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama hicho amesema kuwa CUF ina laani manyanyaso ya Polisi dhidi ya Raia kama ilivyotokea hivi Karibuni Mkoani Kigoma,Tegeta jijini Dar es Salaam, mauaji ya RPC Mwanza, Zanzibar na pia kujeruhiwa kwa waandishi wa habari kwa Risasi kama ilivyotokea Mkoani Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Mtatiro amesema kuwa wanamtaka  IGP  kuwachukulia hatua za Kinidhamu watendaji waliohusika na vitendo hivyo.
CUF  pia imemtaka  waziri wa Nishati na Madini Prf, Muongo kuwaeleza Wananchi ninini Tatizo la kuendelea kwa Mgao wa Umeme kinyemela wakati alikwisha Tangaza kuwa hakutakuwa na Mgao wa Umeme tena.
Aidha Mtatiro amesema kuwa  wanapinga mpango wowote wa kutaka kuongeza bei ya Umeme nabadala yake wameitaka Serikali kutatua tatizo kwenye sekta ya Umeme ili watanzania Wote wanufaike na Huduma hiyo.
MAASINDA, imejaribu   kutafuta  mawazo ya watu wengine wanasemaje juu ya Matamko yanayotolewa na CUF na kufanikiwa kupata ktoka kwa watu mabalimbali ambapo wengi waliisifu kwa matamko yao lakini walitaka waone Vitendo na Sio matamko peke yake.
Josephat  Jacob, ni mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa  CUF kwa mara nyingi wamekuwa wakilaani vitendo viovu vinavyo fanywa na Serikali ya CCM lakini hamna  hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya matamko yao na CUF wanaona kuwa hawajasikilizwa lakini hawachukui hatua zozote.
“Tunataka kuona CUF wanachukua hatua kwani wao wana nafasi ya kusema na kutenda sio wanasema tu, wanalaani tu, na kutoa matamko halafu yasipofanyika wanabaki kimya wanasubiri waseme tena ndipo watoe Tamko na Kulaani tumechoshwa na Siasa zao”, amesema Jacob.

Naye Erick Kivuyo wa Buguruni Dar es Salaam amesema kuwa  Wanataka kuona kuwa hatua zinachukuliwa na sio maongezi  tu ya kuwaridhisha watanzania.
“Maneno Mengi hayavunji  Mfupa watanzania Tunataka kuona jambo linaongelewa na linatendeka sio kuzungumza tu wakati maneno mengi hayavunji Mfupa”, amesema Kivuyo.
Waandishi wa Habari waliokuwemo kwenye Mkutano huo

Hawa ni viongozi wa CUF  waliokuwemo kwenye Mkutano huo

No comments:

Post a Comment