Shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu Afrika, fastjet, leo limeizundua ndege yake ya kwanza
ikiwa nachapa yake kamili, siku mbili tu kabla ya kuanza safari za anga
Tanzania. Kwenye hafla iliyofanyikakwenye uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Julius Kamabarage (JKIA),Dar es Salaam, maafisa wa serikali,
watendaji wa fastjet na wataalamu wa safari za anga walishuhudia ndege
aina ya Airbus A319 ikipaa kwenye anga ya Dar es Salaam kwa mara ya
kwanza.
Kuanzia Alhamisi, 29 Novemba,
fastjet itafanya safari mbili kutwa kwenye ruti zake mbili za mwanzo –
Dar es Salaam-Kilimanjaro na Dar es Salaam-Mwanza, zote zikiwa ni safari
zenye wasafiri wengi wa ndani. Tiketi zilianza kuuzwa wiki mbili
zilizopita na fastjet imeshuhudia mahitaji makubwa, zaidi kuliko
matarajio ya awali. Mpaka sasa idadi ya tiketi zilizonunuliwa ni sawa na
safari 60 za ndege iliyojaa, na mauzo yanaendelea kwa safari za
mwakani. Nauli zitakuwa za wastani wa dollar $80, lakini zinaanzia bei
ya chni kabisa ya $20 kwa safari ya kwenda, kabla ya kodi za serikali
kwa wateja watakowahi kununua tiketi.
Akizungumza mjini Dar es Salaam leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winter, alisema:
“Leo ni siku ya kusisimua sana, na
siyo tu kwa fastjet, bali kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa miaka
mingi tasnia ya safari za anga Afrika imekosa huduma bora, na kulegalega
nyuma ya kwingine duniani. Ustawi wa mapato umeongeza fursa za watu
kuwa na mapato ya ziada, na pamoja na kwamba hilo limeambatana na
mahitaji makubwaya usafiri wa anga, bado watu baraniAfrika wamekosa
fursa za usafiri wa anga wanaoumudu na kuuamini. fastjet sasa itaziba
pengo hilo na kwakuwaletea Watanzania, na hasa bara zima la Afrika,
shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu, likiwa na safari za kituo
hadi kituo, na lenye kujiendesha kwa viwango vya kimataifa vya usalama
na ubora.”
Akizungumzia uzinduzi wa leo, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Airbus – Wateja, alisema:
Uamuzi wa fastjet kujikita kwenye
ndege aina ya A319 pekee ni kidhihirisha ufanisi, kuaminika na kustahili
kwa ndege za aina hiyo kwa ajili ya safari za nauli nafuu barani Afrika
na haswa kusini mwa Jangwa la Sahara. Ndege hiyo itakayotumiwa na
fastjet inaoongoza kwenye mauzo ya ndege aina ya Airbusna inayo safu
mbili za viti,, fastjet imezingatia kuleta viwango vipya vya starehe na
unafuu wa gharamakwenye soko la Afrika ambalo linatarjiwa kuongezeka
mara dufu karikakipindi cha miaka 20 ijayo .”
Fastjet itakuwa ikiendeshwa na
timu yenye uzoefu wa safari za ikiongozwa na Ed Winter, Afisa
Mwendeshaji Mkuu wa zamani wa kampuni ya easyjet na mkurugenzi
mwanzilishi wa shirika la ndege ya bei nafuu la Go, Afisa Biashara Mkuu
Richard Bodin, Mkurugenzi wa zamani wa Mikataba wa easyJet na Mkurugenzi
wa Biashara wa shirika la ndege la bei nafuu la Jet2.com, Mkurugenzi wa
Uendeshaji Rob Bishton, Rubani Kiongozi & Mkuu wa Shughuli za Ndege
wa easyJet na Meneja Mkuu wa Afrika Kyle Haywood, amabye aliwahi kuwa
Afisa Mtendaji Mkuu wa Air Uganda.
Shirika hili la ndege linaendeshwa
chini ya leseni ya chapa ya easyGroup Holdings Limited na Sir Stelios
Haji-Ioannou, mwanzilishi wa shirika la ndege kinara kwa nauli nafuu,
easyJet.
Akizungumzia uzinduzi, Mwenyekiti wa easyGroup Holdings, Sir Stelios alisema:
Sasa ni zamu ya Afrika! Nimefurahi
kuwa nimeshiriki, japo kidogo, kwenye kuanzishwa kwa mapinduzi mengine
tena. Ninawatakia wahusika wote safari njema!”
Shirika hili la ndege linabashiri
kwamba idadi ya abiria wa Fly540, ambayo kwa sasa ni abiria 750,000 kwa
mwaka, itaongezeka mara dufu ndani ya miezi sita kuanzia uzinduzi huu.
Fastjet imepanga ndani ya mwaka mmoja itakuwa na idadi ya ndege 15 aina
ya A319.
Kituo cha kwanza cha fastjet niDar
es Salaam, na cha pili kitakua niNairobi,ambacho kinatarajiwa
kuzinduliwamwakani. Baada ya kujizatiti Afrika Mashariki, shirika hilo
la ndege linatarajia kuzinduliwa Accra, Ghana na Luanda, Angola.
astjet pia inafurahi kutangaza
kwamba leo imetiliana saini mkataba na Swissport International, shirikia
linaloongoza kwenye huduma za sekta ya anga viwanjani, ambapo itakuwa
ikihudumia mtandao wote wa shirika hilo la ndege kwa mahitaji yake
kwenye viwanja vya ndege.
Kupitia makubaliano hayo ya
kipekee ya ubia, Swissport ambayo hutoa huduma mbalimbali kwenye viwanja
vya ndege, itawajibika kwa usambazaji na usaidizi wa mlolongo wa ugavi
kwenye mtandao wote wa fastjet.
Juan Jose Alvez, Makamu wa Rais
Mtendaji wa Uhudumiaji kwenye Viwanja vya Ndege Ulaya, Mashariki ya
Kati, Asia na Afrika alidokeza:
“Swissport ina uzoefu mkubwa wa
kutoa huduma kwenye mfumo wa usafiri wa bei nafuu katika bara laUlaya na
tuko tayari kushirikianakuisaidia kuijenga chapa ya fastjet katika bara
laAfrika, kwa kutumia uelewa na michakato yetu. Ubia huu unahusisha
changamoto zote zinazohusiana na uanzishwaji wa mtandao wa kushughulikia
ndege kwenye viwanja vya ndege na mifumo ya usimamizi, na hivyo ubia
huu ni wa kipekee na unawakilisha aina mpya ya uhusiano kati ya mtoa
huduma na shirika la ndege na kutoa firsa kwaSwissport kuendelea kujenga
mtandao wake Afrika kwa ubia na fastjet.”
Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet Ed Winter alidokeza:
“Swissport ina hadhi inayong’ara
kimataifa na historia ya kutoa huduma bora kwa mashirika ya ndege kwenye
viwanja vya ndege kote duniani. fastjet inajenga shirika la ndege la
bara la Afrika likiwa na viwango vya kimataifa vya usalama, ubora,
ulinzi na kuaminika na hivyo ni muhimu kwetu kuwa na mbia ambaye
atoakipaumbele cha juu kwa viwango vya ubora kulingana na malengo yetu
ya kababmbe ya kustawi barani Afrika.”
No comments:
Post a Comment