Pichani chini ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng.Christopher Sayi (aliyesimama)akifungua Warsha maalum ya Viongozi kuhusu hifadhi ya Mazingira ya
Bonde la Ziwa Victoria katika Hotel ya Golden Crest Mwanza. Warsha hii
inawajumuisha Viongozi mbalimbali toka Wilaya na Mikoa inayozunguka
Bonde la Ziwa Victoria wakiwemo Waheshimiwa Wabunge,Wakuu wa Wilaya
pamoja na Wataalamu wa Maji,Mazingira na Kilimo. Kulia kwake ni BI
Mwamvua Jilumbe Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu..Wa kwanza kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba ambaye alimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhe. Eng.Evarist Ndikilio

Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria Semina hiyo.Kushoto ni Mbungewa Bariadi Mashariki Mhe John Cheyo na wa kwa kwanza kushoto walioketi
ni Mkuu wa Wilaya Meatu Jaquiline Liana
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng.Christopher Sayi akisikiliza kwamakini mada kuhusu utunzaji wa Mazingira katika Semina ya Viongozi
kuhusu hifadhi ya Mazingira ya Bonde la Ziwa Victoria iliyofanyika
katika Hoteli Golden Crest Jijini Mwanza. Kulia kwake ni Mhe. Dr
Kamani Mbunge wa Busega na wa kwanza kulia ni Bi Mwamvua Jilunde
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Warsha hii ni sehemu ya Maadhimisho
ya Siku ya Ziwa Victoria itakafikia kilele chake tarehe 29 Novemba
mjini Bariadi.
Picha zote Nurdin Ndimbe (Wizara ya Maji)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji Eng.Christopher Sayi akiwa katika picha ya
pamoja na wajumbe wa mkutano huo mara baada ya kuufumgua rasmi.
No comments:
Post a Comment