Tuesday, September 18, 2012

NOTI MPYA ZINATENGENEZA MADAWA YA KULEVYA.; VIJANA WENGI WANATUMIA

Noti mpya  amabazo inatumika hivi sasa nchini Tanzania
BAADA ya kuzuka mtindo wa kuzikataa Sarafu za Shilingi 10 na Shilingi 20 kutotumika huku Benki kuu ikikaa kimya, baadhi ya wananchi wameanza kuziharibu kwa makusudi noti za shilingi 500 na 2,000 kwa kuondoa 'ufito' unaong'aa na unaohalalisha pesa hizo na kisha kuutumia katika kutengeneza pombe za kienyeji au bia ili kuongeza kileo wakidai kuwa husaidia kuokoa pesa kwani hulewa kwa muda mfupi.

Wananchi hao pia wanachomoa ufito huo na kuchanganya na sigara au tumbaku ambapo hudai hulewa haraka.

Hali hiyo ambayo imeambatana na uadimikaji wa noti hizo, imeshika kasi eneo la Kijiji cha Maleza, Kata ya Kipeta,Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, vile vile kwenye vijiji vya Kilangawana na Kamsamba.

Wananchi kadhaa ambao hawakupenda majina yao kutajwa, wamethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kuitaka Serikali na Benki Kuu kuchukua hatua za haraka ili kukomesha vitendo hivyo.

Katika hali ya kuhalalisha noti hizo zilizoharibiwa wahalifu hao hutumia gundi kwa kutumia uzi wa mifuko ya mbolea ili ziendelee kutumika.