Chama cha
walimu Tanzani CWT kimeitaka serikali kuacha kuwadanganya kama watoto kufuatia Serikali kuzindua Baraza la pili la
majadiliano ya pamoja kwenye utumishi wa
wa walimu lililozinduliwa jana na
Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Mhe, Nlugo na kuhudhuriwa na wawakilishi wa CWT. Ambapo CWT imesema kuwa
Baraza hilo halina mamlaka ya kutatua migogoro
sehemu ya kazi au migogoro
iliyokwisha jitokeza baina ya Watumishi wa Serikali na Serikali.
Rais wa CWT
Bw, Gratian Mukoba amesema leo wakati anaongea na waandishi wa Habari
kuwa Kazi ya Baraza hilo ni kuishauri
serikali kuhusu njia mbalimbali za kuzuia kutokea kwa migogoro na hiyo ni kwa
mujibu wa kifungu cha Sita cha Sheria ya
majadiliano ya pamoja kwenye utumishi wa umma ya mwaka 2003 pamoja
na kanuni zake za mwaka 2005.
Amesema
kuwa Chombo pekee chenye uwezo wa
kushughulikia migogoro ni Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ambapo chama
kilipeleka mgogoro wake na kufikia hatua ya kutoelewa.
Ameishauri
Serikali kufungua upya jalada la
majadiliano kwani chama kinaamini kuwa walimu wamerudi kazini wakiwa hawana ari
ya kufanya kazi kwani wanasubiri
majadiliano kufanyika kwa ajili ya mwaka
ujao wa Fedha, hivyo ili kuwatia Moyo walimu
na kuwaongezea ari ya kufanya kazi
madai yao yanahitaji kusikilizwa ndani ya mwaka huu wa Fedha.