Kampuni ya Msama Promotions, imekamata watu watatu
wanaotuhumiwa kuuza kazi za wasanii kinyume na taratibu.
Akizungumza na Dira ya Mtanzania, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex
Msama (pichani), alisema kuwa vijana hao walikamatwa katika eneo la
Ubungo jijini Dar es Salaam.
WAlitaja majina ya ya waliokamatwa katika tuklio hilo kuwa ni Malik Sultan, Ally
Msangi, Edward Michael na Sijali Andrew ambao walikuwa na CD feki 322 za
wanamuziki mbalimbali na wasanii wengine.
Msama alisema zoezi la kukamata wezi wa kazi za wasanii
linaendelea kwa kufanya uchunguzi katika maeneo sugu ambako hatua inayofuata ni
kwa wale wanauza kazi hizo mikononi.
Aidha Msama analishukuru Jeshi la Polisi kwa
ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa timu ya vijana wake wanaosaka wezi wa kazi
za wasanii.
|