TAMKO LA TASWA KUHUSU CECAFA
kwa hisani ya www.dinaismail.blogspot.com
CHAMA Cha Waandishi wa Habari
za Michezo (TASWA), kimesikitishwa na hatua ya Baraza la Michezo la Vyama vya
michezo la Afrika Mashariki (CECAFA),
kuwanyanyasa na kuwadhalilisha waandishi wa habari katika mchezo wa
fainali Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kufuatia kudhalilishwa huko
kwa waandishi katika fainali hiyo ya michuano ya kombe la Kagame kati ya Yanga
na Azam, TASWA imelaani kitendo hicho na kuwaondolea utu, udhalilishaji na
unyanyasaji kulikosababishwa na baadhi yao
kutandikwa makofi na askari polisi mithiri ya vibaka.
Waandishi wa habari za
michezo wa Tanzania wamekuwa
wasikivu, waadilifu na watu wanaofuata taratibu, lakini katika fainali hiyo mara baada ya
mchezo walifanyiwa vitendo ambavyo havikulingana na tabia yao.
Lengo la waandishi si kuleta
vurugu bali kuhakikisha wananchi wanapata habari kwa kila tukio lilikuwa
linatokea uwanja, badala yake walionekana hawana thamani mbele ya jamii
inayowawakilisha.
TASWA inalaani kitendo cha
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye kwa kutoa agizo kwa polisi kuwazuia
waandishi kuingia uwanjani kumalizia kazi zao za kuhoji makocha na wachezaji,
hali iliyosababisha vurugu.
CECAFA walijenga urafiki wa
karibu na waandishi kipindi chote cha mashindano hayo na Kagame kwa lengo la
kuyatangaza , lakini mwisho wa yote walionekana kama taulo la deki limekuwa na
thamini pale ambapo linahitajika kwa deki, lakini baada ya hapo halina thamani
tena.
Lakini TASWA inafanya
uchunguzi juu ya tukio hilo, kufuatia baadhi ya
waandishi kuonesha utovu wa nidhamu kama
baadhi ya viongozi wa TFF na CECAFA walivyodai kuwa walionesha vitendo vya
utovu wa nidhamu kwa kutoa maneno ya kashfa na kutaka kumpiga Musonye
Kufuatia hatua hiyo TASWA imechukua maamuzi yafuatayo
1.Kutoandika jambo lolote linahusu Shirikisho la vyama
vya michezo Afrika Mashariki (CECAFA).
2.Kutoandika jambo lolote linahusu mashindano yoyote
yaliyo chini ya CECAFA.
Ili kuweza kufanya kazi pamoja na CECAFA,TASWA inataka
kuombwa radhi na CECAFA kutokana na kitendo hicho na kuwalipa fidia waandishi
ambao wamepoteza vifaa vya vya kazi na wengine kuhalibiwa vifaa vyao.
TASWA inatoa onyo kali kwa
baadhi ya vyama,viongozi na makampuni wenye tabia ya kutotoa ushirikiano na
dharau kwa waandishi wanapokuwa kwenye kazi zao.
|