Mwenyekiti wa TAMPA Bi, Feddy Tesha, akiongea na waandishi wa habari leo katika
ukumbi wa Bluer Pearl Hotel iliyopo jijini Dar es salaam.
Chama cha Usindikaji wa maziwa Tanzania TAMPA kimeiomba
serikali ipunguze kodi katika usindikaji wa maziwa ili kuonngeza idadi ya
Watanzania wanywa maziwa. Akizungumza katika
Semina YA Wadau wa Usindikaji wa maziwa Mwenyekiti wa Chama hicho alisema
kuwa ni asilimia 43 tu ya watanzania
ndio wanakunywa maziwa yaliyosindikwa kwa sasa jambo ambalo alisem a kuwa hao
ni watu wachache ukilinganisha na maziwa mengi yanayozalishwa Tanzania.
|