Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar
Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya
Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya
Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati, baada ya kutoka
suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri
na wa kuvutia kwa timu zote uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo hivyo
kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.
Wachezaji wa simba pamoja na kocha wao wakipiga picha ya pamoja na kombe lao walilokabidhiwa. | | | | |
|