Katibu
mwenezi wa CCM, Tawi la Nyakasangwe Bw, Benjamin Steven akisistiza jambo wakati
alipokuwa akiongea naWaandishi wa habari juu ya unyanyasaji wao dhidi ya
Polisi.
|
Mjumbe wa
Kijiji cha Nyakasangwe, Jastin Frank, akisisitiza jambo kuwa hawawezi kukubali
kunyanyaswa na polisi wanaotokea kuwanyanyasa hapo kijijini kwao wilayani
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
|
Wanakijiji wa
Nyakasangwe Kata ya Wazo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam wanaiomba serikali iwaangalie na kuwasaidia kuondokana na
unyanyasaji wanaoupata Dhidi ya Polisi wa kupigwa pamoja kufukuzwa katika
maeneo yao huku wakiwaambia kuwa wao ni wavamizi katika maeneo hayo.
Wakizungumza na waandishi wa habari
kijijini hapo wanakijiji hao walisema kuwa wamechoka kuishi kwa
kunyanyaswa na polisi bila ya makosa yoyote kwani wanaishi kama digidigi
(pasipo kulala) na Kisingizio cha wao kunyanyaswa ni kwamba hawatakiwi
kuishi kwenye maeneo hayo kwakuwa wao si wamiliki halali.
Majengo Majengo ni Mwenyekiti wa
kijiji hicho ambapo alisema kuwa Polisi wanakuja kila kukicha kutaka kuwakamata
kwa kisingizio kwamba wanakijiji wote wanaoishi maeneo yale ni wavamizi.
Hata hivyo Majengo alisema kuwa,
Kesi yao ipo mahakamani na inasubiriwa kutolewa hukumu lakini wanashangaa bado
wanakamatwa ovyo na kubambikiwa kesi.
“Kesi yetu hii ipo mahakamani lakini
tunashangaa tunazidi kuwindwa na watu wachache, wakishirikiana na
Polisi”,alisema Majengo.
Alisema kuwa, Askari hao
wanapokwenda kuwakamata, wanatembea na watu watatu wanaodai kuwa msitu wa
kijiji hicho ni maeneo yao.
Aliwataja watu hao kuwa ni,Datsan
Okololo, Omary Ponchi pamoja aliefahamika kwa jina moja tu la Mwamasika
ambao alidai kuwa ndio wanaoshirikiana na askari wa jeshi la polisi kuwakamata
watu kwa madai ya kuwa wao ndio wamiliki halali wa msitu huo wa kijiji hicho.
Naye Katibu Mwenezi wa
CCM Tawi Nyakasangwe Benjamin Steven, alisema kuwa viongozi wenzake
wote wamekamatwa na polisi na Mpaka sasa Mwenyekiti wake hajulikani alipo baada
ya kukimbia askari walipotaka kumkamata.
Akielezea kukamatwa huko kwa
viongozi wenzake alisema kuwa, baada ya uchaguzi uliofanyika tarehe
tano mwezi huu yalikuja magari mawili ya polisi(Defender) zilizofunikwa
na vitambaa vyeusi kwenye ubao wa namba na kuwakamata viongozi wao kwa makosa
ya Uvamizi.
“Mimi nashangaa Maswala ya Uvamizi
yanaingiliana vipi na Chama, naomba jeshi la Polisi lisichanganye mambo, kwa
mambo ya Uvamizi yanamuhusu mwenyekiti wa kijiji na serikali yake na hayawezi
kuhusiana na Chama hata siku moja”, alisema Benjamin Steven.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya
Kinondoni Jordan Rugimana alipoulizwa kuhusiana na sakata hili alisema
kuwa kuhusiana na wannchi hao kunynyaswa na kubomolewa nyumba zao kwa kosa la
uvamizi ni swala la Mahakama ndiyo itakayotoa majibu kama wanakijiji hao
wanauhalali wa kuishi maeneo hayo au la.
Aidha, kamanda wa polisi mkoa wa
kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alipoulizwa kuhusiana na swala hilo alisema
kuwa, huo ni mkakati wa jeshi la polisi kuendelea kuwakamata wavamizi wa maeneo
ya watu.Hizi ndizo namba zao 0714356974,0714573564