Friday, July 20, 2012

AJALI YA KUZAMA KWA MELI ZANZIBAR, CUF WATUPIA LAWAMA VIOKOSI VYA ULINZI NA UOKOAJI

Mwenyekiti wa Chama cha wananchi  CUF  Profesa Ibrahim Lipumpa akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam juu ya Ajali ya Kuzama kwa Meli ya MV Skagit ya Kampuni ya Seagul na Maafa ya Abiria  waliozama na Kufa Maji iliyotokea Tarehe 18/08/2012. Ambapo alitoa lawama kwa Vikosi vya ulinzi na kusema kuwa  vilikosa kutimiza  wajibu wao kwa wakati, kwa mfano kikosi cha KMKM kilifika katika eneo la tukio saa 12 jioni wakati kikosi cha wanamaji cha JWTZ kilifika katika eneo la tukio  siku ya pili yake jambo ambalo  ilisababisha  watu wengi kufa kwa kukosa masaada wa kuokolewa. Aidha alisema kuwa Chama kinawasiwasi na manahodha  na Mabaharia katika kujua uwezo wa chombo chao kama kina uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa  kwa siku husika kwa siku husika. “Tunawasiwasi na manahodha pamoja na Mabaharia na Pengine hata SUMATRA na wakala wa meli Zanzibar  ZMA haina sifa sahihi za manahodha na Mabaharia hawa.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo.