Wednesday, June 13, 2012

UNDER THE SAME SUN YATANGAZA MAUAJI MENGINE YA ALBINO YALIYOTOKEA ARUSHA.

Afisa utetezi wa matukio ya mauaji  ya Albino kutoka Shirika la Under the Same Sun Bw, Kondo Seif akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za Shirika hilo linalohusika na kutetea Maalbino nchini juu ya mauaji ya Albino yanayoendelea kutokea nchini Tanzania. Bw, Kondo alisema kuwa wanasikitika na kufadhaishwa na mauaji ya mwanaume asiyetambuliwa kati ya umri wa miaka 25-35 mwenye ulemavu wa ngozi yualiyofanyika  katika kijiji cha nambala kata ya Kikwe Tarafa ya Mbuguni  wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha . Alisema kuwa wamekuta mwili wake ukiwa umeharibiwa vibaya na kwamba ulikuwa umen'golewa sehemu kadha za viungo vya mwili wake vikiwemo mikono, masikio, ulimi,ngozi ya usoni,sehemu za makalio na sehemu zote za nyeti zake na nywele za kichwani. Alisema kuwa mwili wake umehifadhiwa katika hosipitali ya Mkoa Mount Meru.

 Afisa katika shirika la Under The Same Sun Bw, Gamanyo Mboya, akikazia unyanyasaji huo unaofanyika na watu wasiojulikana na alisema kuwa kuanzia january kufikia machi mwaka huu tayari wamepokea matukio sita ya kikatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo alisema kuwa kwasasa walemavu wa ngozi wamekuwa wakisafirishwa nje ya nchi na kwenda kuuawa alithibitisha hayo kwakusema kuwa walipata taarifa ya mtoto mwenye umri wa miaka 3 akisafirishwa kutoka Tanzania na kupelekwa  Bukinafaso.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini.