Wednesday, June 27, 2012

TCU YAKUTANA NA WANAFUNZI KUTOKA VYUO MBALIMBALI NCHINI KUJADILI NAMNA YA KUTATUA CHANGAMOTO VYUONI

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo vikuu nchini Prph Sifuni Mchome akizunngumza na waandishi wa habari wakati   wa mazungumzo na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini ambapo alisema lengo lao ni kkujadili changamoto mbalimbali zinazowakumba wanafunzi wawapo vyuoni na namna ya kuzitatua ambapo alisema kuwa mpaka sasa tayari kuna wanafunzi 40,000 walioomba kujiunga na Elimu ya Chuo kikuu jambo ambalo limewafanya wafikirie kuongeza vyo kutokana na muamko wa wanafunzzi kutaka Elimu. Alisema kuwa mpaka sasa wanavyuo vikuu 49 na pia kwa wanafunzi wengine walio omba chuo kupitia TCU watapangwa kwenye vyuo vya Binafsi kutokana na Uhaba wa Vyuo.Mkutano huo umefanyika leo katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam

Prof  Sifuni akisikiliza kwa makini maswali kutoka kwa baadhi ya wanafunzi kutoka vyuombalimbali nchini waliowawakilisha wenzao.

Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria kwenye mkutano huo.