Mkurugenzi
mkuu wa Nabaki Africa Ltd Bw, Hamish Hamilton akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa kukabidhi hundi ya kiasi cha shilingi 15,000,000, kwa mshindi
wa droo iliyochzeshwa na kampuni hiyo may 31 mwaka huu. Nabaki Africa
ilikabidhi hundi hiyo kwa Bw, Kalembo Bisaya ambaye ndiye mshindi wa Droo hiyo
ambapo kila mmoja wa wateja walioshiriki shindano hilo alinunua aidha vifaa vya mfumo wa
kuvuna maji ya mvua vijulikanavyo kama Marley Gutters au mfumo wa kuzuia
joto katika paa pamoja na vigae vya kuezekea aina ya DECRA. Washiriki
katika shindano hilo walikuwa jumla ya washiriki 101 ambapo amesema wateja
wote ambao wamenunua vigae vya DECRA wataweza kuangalia juu ya mapaa yao na
kuona tofauti nzuri ambayo ni DECRA halali tu ndiyo inatoa. Makabidhiano hayo ya
hundi yalifanyika katika makao makuu ya Nabaki Africa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
mkuu msaidizi wa Nabaki Africa Ltd Bi Tamia Hamilton akifafnua juu ya
utoaji wa zawadi hizo kwa wale wateja waliofanikiwa kushinda katika Droo hiyo.
Mkurugenzi
mkuu msaidizi wa Nabaki Afrika Ltd Bi Tamia Hamilton (kulia) akimkabidhi
mfano wa hundi wa kiasi cha Tsh, 15,000,000/= Bw, Kilembo Bisaya baada ya kushinda katika
droo iliyochezeshwa na kampuni ya Nabaki Afrika LTD .
Mshindi
wa Droo hiyo Bw, Kalembo Bisaya akizungumza na waandishi wa habari juu ya
furaha yake baada ya kukabidhiwa hundi hiyo.
Bwana Alison Malopa akifafanua namna ya utoaji wa zawadi baada ya kuelezewa na wakurugenzi kwa lugha ya kingereza.
Mshindi wa droo Bw, Kilembo Bisaya akiwa kwenye picha ya pamoja na mkewe baada ya kupewa hundi yake.