Friday, June 29, 2012

ILALA YAANZA RASMI OPERESHENI YA KUWEKA MAZINGIRA YAO KATIKA HALI YA USAFI, YATUMIA MAGARI MAALUM KUFAGIA BARABARA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe, Said Meck Sadick (katikati) na kushoto kwake ni Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe, Jerry Slaa kwa pamoja wakikagua baadhi ya vifaa vya usafi leo jijini Dar es Salaam ambapo hayo ni moja ya maonyesho ya kuweka Manispaa ya Ilala katika hali ya usafi. Katika maonyesho hayo kulikuwepo naq Magari maalum makubwa(malori)kwa ajili ya kufanyia usafi barabarani road sweeper ambapo Mkuu wa mkoa alisema kuwa kutokana na Tecknolojia hiyo anaimani kuwa usafi unawezekana Dar es Salaam.

Moja ya gari maalum kwa ajili ya kufagia barabara (Road sweeper) gari hilo linafagia barabara na kumwaga uchafu mbali zaidi.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe, Said Meck Sadick akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Operesheni ya usafi inayoendelea katika Manispaa ya Ilala ambapo aliwataka wananchi wa ilala kuwa na Ushirikiano kwa kutoegesha magari ovyo pasipo utaritibu ili waweze kupisha magari ya kufanyia usafi.