Mama Salma Kikwete Mke wa
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi
wa Kampeni ya STAND UP FOR AFRICAN MOTHERS iliyoandaliwa na AMREF ambapo
aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kupunguza vifo vya kinamama wajawazito
na watoto wao wakati wa kujifungua, Mama salma alisema kuwa kila mwananchi
akichangia Sh.1000 za kitanzania, zitasaidia kusomesha wakunga 4222
watakaotumika kuwauguza wamama wajawazito pindi wanapokuwa kwenye kipindi cha
kujifungua, Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Dk Hussein
Mwinyi akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi huo ambapo aliitaka Amref isaidie
kukusanya pesa kutoka kwa nanchi pamoja ana Makampuni Binafsi ili fedha za
kusomesha wakunga zipatikane
Baadhi ya Wafanyakazi wa
Amref wakisherehekea kwenye uzinduzi huo
Mama Salma Kikwete
akimpongeza Mkurugenzi mkuu wa Amref Dk Festus Ilako kwa kuonyesha upendo kwa
kinamaama wajawazito.
Kikundi cha Burudani kutoka
Mjomba Band kikifanya mambo kwenye Uzinduzi huo.