Thursday, May 9, 2013

WAMILIKI WA KAMPUNI WATAKIWA KUZALISHA KWA KUJALI MAZINGIRA NA AFYA ZA BINADAMU NI AGIZO WAKATI WA SEMINA YA TBS NA SHIRIKA LA VIWANGO LA KIMATAIFA

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania TBS akijadiliana jambo na  Mkurugenzi wa Masoko katika Wizara ya Viwanda na Bihashara Mhe, Odilo Majengo katika Semina iliyoandaliwa na TBS pamoja na Shirika la Viwango la Kimataifa iliyofanyika leo katika Hoteli ya Bluer Pearl Jijini Dar es Salaam.
 Mashirika na Makampuni Mbalimbali nchini Tanzania wametakiwa kuzalisha Bidhaa zao kwa kujali mazingira na kujali afya za Binadamu wengine.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Masoko katika Wizara ya Viwanda na Bihashara Bw, Odilo Majengo, katika Warsha iliyoandaliwa na TBS pamoja na Shirika la Viwango la Kimataifa  yenye lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na viwango vizuri katika Bidhaa zake pamoja na  Mazingira mazuri ili kulinda Afya za Binadamu.

"Nilazima Makampuni na Mashirika yanazalisha kwa kutunza Mazingira pamoja na  kujali Afya za Binadamu wanaozunguka katika Kampuni hiyo", Amesema Bw Majengo.
Mgeni Rasmi Katika Semina hiyo Bw, Odila Majengo akiwa kwenye Picha ya Pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria katika Warsha Hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko katika Wizara ya Viwanda na Bihashara Bw, Odilo Majengo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Warsha hiyo.


Kaimu Mkurugenzi wa TBS akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa Warsha hiyo.

No comments:

Post a Comment