Thursday, May 9, 2013

TRA YAKUTANA TENA NA WAFANYA BIHASHARA YA KUUZA VIFAA VYA UJENZI

Mwelimishaji Mwandamizi wa TRA Bi Alvera Ndabagoya akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa Semina iliyowakutanisha TRA na wafanyabihashara wa Vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuwapa Elimu juu ya ulipaji kodi kwa njia ya Kielektoniki ambapo amesema kuwa Mfumo huo ni awamu ya pili ikiwa awamu ya Kwanza iliwahusisha wafanyabihashara wakubwa waliokuwa wanazalisha kuanzia kiasi cha shilingi milioni 40 nakuendelea.
 Bi, Ndabagoya amesema kuwa, Awamu hii ya Pili itawahusisha wafanyabihashara wanaozalisha kati ya shilingi milioni kumi na tano hadi 40 ambapo Mfumo huu unatarajiwa kuanza kutumika kuanzia May 5 mwaka huu.
Mwelimishaji Mwandamizi Mkuu wa TRA akijibu swali kutoka kwa wafanyabihashara

Hawa ni baadhi ya Wafanyabihashara tu waliohudhuria katika Warsha hiyo

No comments:

Post a Comment