Wadau watafiti wa Maswala ya Ajira na Kazi wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja baada ya Mkutano uliokuwa unajadili kuhusu kufanya Utafiti wa Maswala ya Ajira na Kazi. |
Wadau wa
tafiti wa hali ya nguvu kazi na ajira nchini Tanzania wamekutana katika mkutano leo uliofanyika katika Hoteli ya Peacok
jijini Dar es salaam mkutano wenye lengo la kujadili kwa pamoja upatikanaji wa
ajira nchini na kupanga jinsi ya kufanya tafiti juu ya upatikanaji wa ajira
nchini.
Akisoma
hotuba ya katibu mkuu wa wizara ya kazi na ajira mwakilishi wake katika
ufunguzi huo Bw Ally Ahmed amesema Tanzania bado inapita katika kipindi kigumu sana
katika maswala ya ajira hususani kwa vijana hivyo ni lazima watafiti mbalimbali
wajitokeze kufanya tafiti na hatimaye kutoa sulihisho la upatikanaji wa ajira
nchini
Ameongeza
kuwa nchini Tanzania zaidi ya asilimia 75.1 ya watu wenye uweo wa kufanya kazi
wanajihusisha na shguhuli zilizo katika secta isiyo rasmi.
Aidha
amewaomba wadau hao wa tafiti kuhakikisha wanajadili kwa pamoja na baadae
kutoka na tafiti ambazo zitasaidia kuondokana na tatizo la ajira nchini huku
akiahidi serikali kuwasaidia kwa hali na mali kuhakikisha wanafanikiwa katika
suala hilo
Kwa
mujibu wa wadau hao maeneo muhimu watakayoyajadili na mwishoni kuyafanyia
tafiti ni hali ya ajira nchini,hali ya kipato nchini,pamoja na hali ya ajira
kwa watoto.
Wakiwa pamoja katika Pozzz |
No comments:
Post a Comment