Katika
tukio lisilo la kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa
mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya
kitaifa ambapo kwa busara za watendaji wa ITV waliwaalika wasemaji wakuu
wa mjadala huo kuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya Siasa wakianza na
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana naKatibu Mkuu wa CDM Ndugu Slaa.Kutokana
na hudhuri wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri
kuelekea Dodoma kwenda kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa
na majukumu mengine muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa
Itikadi na Uenezi CCM,ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo wa viongozi wa vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na mustakabali wan chi yetu.Baada
ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni asubuhi ya Leo, Nape
pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa atamuwakilisha Katibu
Mkuu wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya kusikia kauli hiyo, Dr
Slaa alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa sababu
anamtaja vibaya kwenye mikutano yake.Hata
busara zilipotumika za kumsihi apungumze munkari na kumtaka kuangalia
umuhimu wa mazungumzo hayo na kipindi hicho kwa watanzania, bado Slaa
aligoma na kuondoka katika ofisi za ITV
No comments:
Post a Comment