Friday, May 24, 2013

TENDA ZOTE ZA SERIKALI SASA KUPEWA WAKANDARASI WAZALENDO NA SIO WACHINA TENAAAAAA

Waziri wa Ujenzi Prof John Magufuli, akizungumza wakati akifunga Maonyesho ya Bodi ya Wakandarasi leo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo amsema kuwa Serikali itakuwa inawapa Kipaombele Wakandarasi wazalendo katika Tenda zote zitakazokuwa zinatokea Serikalini badala ya kuwapa Wakandarasi wa Kigeni kama ilivyokuwa Mwanzo.
 Amewataka Wakandarasi endapo watapewa Tenda za Nchi wajiepushe na vitendo vya Rusha na Badala yake kuonyesha Uzalendo wao katika Nchi yao.

Prof Magufuli amesema kuwa, endapo Mkandarasi atabainika kujihusisha na Vitendo vya Rushwa basi atachukuliwa hatua Stahiki.
Baadhi ya Makandarasi wakimsikiliza Prof Magufuli kwa Makini.



No comments:

Post a Comment