Eng Stephen Minja ambaye ni Afisa Mhakiki kutoka TBS akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa Maonyesho ya Bodi ya Wakandarasi Tanzania.
|
Shirika la Viwango Tanzania TBS limewataka Wakandarasi wote
Tanzania, kuwa na uhakika na Vifaa vya Ujenzi wanavyovitumia ili kuepusha
Athari inayoweza kujitokeza baada ya Kazi yao.
Akizungumza katika Maonyesho ya Bodi ya Wakandarasi Afisa
Mhakiki Viwango kutoka TBS Eng Stephen Minja amesema kuwa, ni vyema Wakandarasi
wakakagua vifaa vyao kabla ya kuvitumia ili kuhakiki Ubora wa vifaa hivyo na
kama vipo katika viwango sahihi.
Eng Minja amesema kuwa, kama Mkandarasi atakuwa na wasiwasi
na vifaa vyake ni vyema akawasiliana na tbs ili wakakague wenyewe kupitia
wataalamu wake.
Ameendelea kusema kuwa, Shirika la Viwango litahakikisha
kuwa vifaa vya ujenzi vinavyotumika katika Ujenzi
vinakuwa katika kiwango Stahili ambapo Endapo TBS itabaini kuwa kuna Kiwanda kinachozalisha
Vifaa ambavyo havipo katika viwango Basi hawatasita Kukifungia Kiwanda hicho.
Ameongeza kuwa tayari Mpaka sasa wameshazifutia leseni
Viwanda sita ambavyo vilikuwa vinazalisha Bidhaa ambazo sio stahili, na ametaja
Viwanda hivyo kuwa ni Viwanda vitano vya Nondo vilivyokuwa vinafanya Shughuli
zake Jijini Dar es Salaam, pamoja na Kiwanda kimoja cha Maji kilichopo Mkoani
Tanga.
Aidha Eng, Minja amesema kuwa wanampango wa kufanya Msako wa
kushutukiza katika viwanda vinavyozalisha Mabati ili kuchunguza kuwa ni viwanda
gani ambavyo havizalishi Mabati yaliyopo katika Kiwango, na endapo watabaini
basi watakifungia kiwanda Husika.
Hapa akijibu swali kutoka kwa Waandishi wa habari |
No comments:
Post a Comment