ASKARI POLISI MSTAAFU SAMSON BWIRE AKIWA AMEFIKISHWA HOSPITALINI MDA
MCHACHE BAADA YA KURUKA KUTOKA KWENYE GARI AKIJARIBU KUKIMBIA.
Mkazi
wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson
Bwire (54), anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake
Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi.
Tukio
hilo limetokea jana jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke
wake Happiness Elius (28) huku akiwa
amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto
Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.
Kwa
mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba
walipoenda walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia
ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.
Imefafanuliwa
kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku
wakiomba msaada kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa
kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani.
Majirani
kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha
koplo kwa nia ya kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada
kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.
Hata
hivyo Wakati gari la Poisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la
Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo
kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.
Mtoto
Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama
kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.
MATUKIO KATIKA PICHA
MTOTO WA MIAKA 4 DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI KWA HUDUMA AYA KWANZA.
HAPA AFANDE AKIWA HOI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI..
MADAKTARI WAKIJITAHIDI KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.
MADAKTARI WAKIWA KAZINI KUHAKIKISHA WANAOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.
AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI HUKU AKIWA AMEFUNGWA PINGU.
No comments:
Post a Comment