Kiongozi wa Mila wa kabila la
Wamasai Justin Nokoren (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, Dar
es Salaam leo, wakati viongozi wa mila na wananchi wa Ngorongoro
walipokuwa wakielezea mgogoro wao wa ardhi na Serikali katika Tarafa ya
Loliondo, wilayani Ngorongoro. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Ololosolarm,
Yannick Ndoinyo wa Kata ya Arash, Mathew Silon.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wa Wilaya ya Ngorongoro
wameapa kufia katika ardhi ya wilaya hiyo badala ya kumuachia
mwekezaji wa Kampuni ya Otterlo Business Corapation (OBC), kama serikali
inavyotaka.
Hayo yalisemwa na Diwani wa Kata ya
Olosokwani Yamick Ndoinyo wakati akizungumza na waandisghi wa habari Dar
es Salaam jana huku akiwa na wajumbe wengine kutoka katika wilaya hiyo
kuhusu mgogoro wa ardhi ya Loliondo na kutoa maazimio kwa serikali.
"Kwa niaba ya wananchi wa Loliondo
pamoja na viongozi wetu tunaitaka Serikali iache mara moja mpango wake
wa kugawa ardhi ya vijiji vyetu kwa manufaa ya mwekezaji kwa kisingizio
cha manufaa ya umma badala yake itambue ardhi yote ya Loliondo ni mali
ya vijiji hivyo iviachie vijiji kujipangia matumizi yao ya ardhi kwa
njia shirikishi na mujibu wa sheria za ardhi" alisema Ndoinyo.
Alisema serikali isipo badilisha
msimamo wake wake wananchi wa Ngorongoro kwa umoja wao watalilinda ardhi
hiyo kwa njia zozote zile kwani ndio uhai wao.
Ndoinyo aliendelea kutabainisha kuwa
serikali inatakiwa kuacha kupotosha umma kwamba ardhi hiyo siyo ya
vijijni na ieshimu sheria kwa kuvipa vijiji haki yao ya kujiamulia mambo
yao yenyewe kwa kutumia sheria zilizopo za ardhi na za serikali za
mitaa.
Ndoinyo alisema serikali inatakiwa
kuacha vitisho kwa wananchi wa Loliondo na wawakilishi wao,
wanaharakati, mashirika na waandishi wa habari wanaoufatilia mgogoro
huo.
Naye Diwani wa Kata ya Soistan Daniel
Ngoitiko alisema serikali kuendelea kuyatisha makundim hayo inakiuka
haki ya kikatiba ya kupata habari na kuzuia jamii kuelimishwa juu ya
haki zao za kikatiba na kisheria kwa manufaa yao wenyewe na taifa kwa
ujumla.
"Kuendelea kufanya hivyo ni kuwanyima
haki yao ya kupata taarifa na kutoa maoni kama inavyolindwa na katiba
ya Tanzania na mikataba ya Kimataifa ambayo serikali imeridhia" alisema
Ngoitiko.
Maazimio hayo yamefikiwa na viongozi
wa vijiji na Kata za Ololosokwan, Malambo, Olorien. Soitsambu na Arash
na vijiji vya Piyaya, Soitsambu, Oloirien, Arash, Malambo na Ololosokwan
kwa niaba ya wenzao ambao hawakufika Dar es Salaam.
Mgogor huo umeibuka baada ya machi 21
mwaka huu Waziri wa Maliasikli na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kutoa
taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari kuwa wizara hiyo
inabadilisha mipaka na ukubwa wa eneo la pori tengefu la Loliondo
kutoka kilometa za mraba 4,000 hadi 1500.
Katika taarifa hiyo Waziri
alitangazia umma kwamba Serikali imeamua kupunguza ukubwa wa eneo hilo
ili kutatua migogoro iliyopo kataika eneo hilo, kunusuru ikolojia ya
hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro na Pori tengefu la Loliondo.
Mgogoro katika eneo hilo la Loliondo
umedumu kwa muda mrefu na inaanzia mwaka 1992 wakati serikali ilipoingia
katika mkataba na Kampuni ya Otterlo Business Corapation ya kutumia
ardhi za vijiji bila ya kushirikisha vijiji na bila ridhaa yao.
No comments:
Post a Comment