Friday, April 19, 2013

TANGAZO KUTOKA BARAZA LA MITIHANI,MITIHANI YA QT NA KIDATO CHA NNE

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia Watahiniwa wote wa Kujitegemea wanaotarajia kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) na Kidato cha Nne (CSEE) Mwezi Novemba 2013 kwamba Usajili utafungwa rasmi tarehe 30/4/2013.

Baraza la Mitihani linasisitiza kuwa hakuna mtahiniwa atakayesajiliwa baada ya tarehe 30/4/2013. Hivyo watahiniwa ambao bado hawajajisajili hadi sasa wanashauriwa kujisajili mapema iwezekanavyo kabla ya usajili kufungwa.  Usajili unafanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz.

IMETOLEWA NA:

KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

No comments:

Post a Comment