Na Mwandishi Wetu, Tanga
MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF),
awametaka wananchi wa mkoa wake kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika
shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Kauli hiyo aliitoa kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza
katika ziara yake hiyo katika kata za halmashauri ya jiji la Tanga na Wilaya ya
Pangani, ambapo alisema ni muhimu kwa kila mwanajamii kutambua wajibu wake.
“Suala la amaendeleo halina itikadi na sasa sio wakati wa
kampeni za uchaguzi, ni jukumu letu kwa viongozi wa Mkoa wa Tanga, kuhakikisha
tunashiriki katika miradi ya maendeleo kwa dhati.
“Ni wazi Mkoa wa Tanga tuna kila sababu ya kuhakikisha
tunaimarisha uchumi wetu hasa baada ya miaka kadhaa viwanda vyake kufa kutokana
na kutokuwepo na usimamizi mzuri. Ikiwa kila mtu atatambua wajibu wake ni wazi
tutafanikiwa kufikia lengo letu,” alisema Mwidau.
Alisema kutokana na hali hiyo kila mara amekuwa
akishiriki katika kuhamasisha maendeleo katika maeneo yote ya mkoa huo bila
kujali uongozi wa kaa upo chini ya chama cha CUF au CCM.
“Tanga tuna ardhi nzuri na tuna kila sababu ya
kujivunia jambo hili ingawa kukosekana kwa usimamizi madhubuti kwetu
imekuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi wetu tunaowaongoza, wabunge wote wa mkoa
huu tuna wajibu wa kuliangalia hili,” alisema Mbunge Mwidau.
Katika ziara hiyo akiwa wilayani Pangani Mwidau, alisema
kuwa amefurahishwa kuona wananchi na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwera
kuamua kuchimba kisima kikubwa zaidi ya kilichopo sasa na katika hilo
amefurahishwa kuona mchango wa awali wa mashine aliyoitoa imewezesha kujengwa
kwa kisima kisima kingine kikubwa cha futi 45 na kipenyo cha nchi sita.
Mbunge Mwidau akisalimia na wanawake wa kikundi cha
wajasiriamali wafugaji wa kuku wa Kata ya Pongwe kijiji cha Marizara.
|
Mbunge Mwidau akikabidhi mifuko kumi ya saruji kwa Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Msambweni Bahati Marungu kwa ajili ya ujenzi shule ya
Sekondari ya Kata ya Msambweni.
|
No comments:
Post a Comment