Hii
ndiyo gari inayotumika na mafundi wa Tanesco kupita nyumba hadi nyumba
kukagua mita zao kama zimechezewa na kulitia hasara shirika hilo
Zaidi
ya shilingi milioni 50 zimetajwa kupotea katika shirika la umeme tanesco mkoani
mbeya kwa kipindi cha miezi 3 kufuatia kuibuka kwa wimbi la wizi wa mafuta ya
transifoma pamoja na wizi wa vifaa vingine .
Meneja
wa shirika hilo mkoa wa mbeya Mhandisi Simon Maganga amesema kuna tatizo kubwa
la wizi wa transifoma na mafuta yake pamoja na vifaa vingine ambavyo thamani
yake inakadiliwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 50 vimeibiwa katika kipindi
hicho .
Amesema
suala la wizi limeibuka upya ambapo baadhi ya wananchi wasio kuwa waminifu
wamekuwa wakifanya vitendo hivyo hasa kwa maeneo ya wilayani ambako ndiko wizi
huo umekuwa ukifanyika marakwa mara.
Kufuatia
hali hiyo tayari shirika hilo limekwisha patiwa vifaa ambavyo vitaweza
kuwasaidia katika msako huo wa kuwakamata wahalifu wanao lihujumu shirika hilo.
Moja
ya vifaa vipya vilivyotolewa na serikali katika kukabiliana na tatizo hilo
Mhandisi Maganga amesema kuwa ni pamoja na vyombo vya usafiri ambavyo teyari
wamekwisha patiwa gari jipaya aina na Toyota Landcruse ambayo itawalahisishia
kufika maeneo mengi zaidi .
Hata
hivyo Meneja huyo amesema kuwa kutokana na msako waliokwisha kuanza
wamefanikiwa kuwakamata baadhi ya wahalifu wanaolihujumu shirika hilo na
wanatalajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.
Ametaja
baadhi ya wilaya ambazo zimekuwa vinara wa wizi huo amabyo ni pamoja na
Halimashauri ya wilaya ya Mbarali pamoja na Mbeya mjini ambapo Apri 12 mwaka
huu walifanikiwa kumakata mkazi wa eneo la Sae Ndugu Saimon Chengula mara baada
ya kujonganishi umeme kinyemela.
Kufuatia
hali huyo ametoa wito kwa wananchi jijini humo na maeneo ya irani kuhakikisha
wanatoa ushirikiano kwa viongozi wa shirika hilo kwa wale ambao wamekuwa
wakilihujumu shirika hilo ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.
|
No comments:
Post a Comment