Tuesday, April 16, 2013

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC NA MAMLAKA YA MAFUNZO YA UFUNDI STADI VETA ZA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la 
Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu (kushoto) na 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mafunzo ya 
Ufundi Stadi (VETA), Zebadiah Moshi 
wakisaini hati za makubaliano.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la 
Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu (kushoto)
akimuangalia Mkurugenzi wa Mamlaka ya 
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Zebadiah Moshi 
(kulia), wakati akisaini hati za makubaliano.
Nyuma yao ni Meneja wa Huduma kwa 
Jamii wa NHC, Muungano Seguya.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la 
Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu (kushoto) na 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi 
Stadi (VETA), Zebadiah Moshi, wakibadilishana
 hati Dar es Salaam leo, baada ya kutiliana 
saini makubaliano ya utoaji wa mafunzo 
kwa vijana ya utumiaji wa mashine za 
Hydraform kujenga nyumba za gharama nafuu.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi 
Stadi (VETA), Zebadiah Moshi (kulia), akitoa hutuba
 fupi kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la 
Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu (kushoto), 
akihutubia kwenye hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa meza kuu wakiwa 
kwenye hafla hiyo.
Vijana watakaopata mafunzo hayo wakiwa katika 
picha ya pamoja na watendaji wakuu wa NHC na VETA.
Vijana watakaopata mafunzo hayo wakiwa katika 
picha ya pamoja na watendaji wakuu wa NHC na VETA.
Mkufunzi wa matumizi wa mashine za Hydraform 
kutoka Afrika Kusini, Henry Cockcroft (kushoto), 
akielekeza jinsi mashine hiyo inavyofanyakazi.
Mkufunzi wa matumizi wa mashine za Hydraform 
kutoka Afrika Kusini, Henry Cockcroft (kushoto), 
akimbidhi kitabu chenye matumizi ya mashine hiyo  
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa 
(NHC), Nehemia Kyando Mchechu.
Mkufunzi wa matumizi wa mashine za Hydraform 
kutoka Afrika Kusini, Henry Cockcroft (kushoto), 
akimbidhi kitabu hicho Mkurugenzi wa Mamlaka ya 
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Zebadiah Moshi.
Vijana watakaopata mafunzo hayo wakipiga makofi
 kufurahia mpango huo.


Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limeingia mkataba na Chuo cha Ufundi Stadi (Veta), wa mafunzo maalumu kwa wanafunzi wa chuo hicho ambao watashiriki katika ujenzi wa nyumba za bei nafuu zinazojengwa na shirika hilo maeneo mbalimbali kwa kutumia matofali ya kisasa.

Mkataba huo umefanyika Dar es Salaam leo ukishirikisha viongozi wa NHC na wakufunzi wa Veta kwa niaba ya wanafunzi hao.

Kwa mujibu wa mkataba huo, wanafunzi 35 wamechaguliwa kushiriki mafunzo hayo kwa vitendo, ambapo watashiriki kufyatua matofali kwa kutumia mashine maalumu za umeme na ujenzi wa nyumba hizo utafanyika katika mikoa 14 nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu, alisema lengo la kuandaa programu hiyo ni kuhakikisha shirika linanufaisha vijana wanaohitimu mafunzo ya ujenzi na kuingia katika soko la ajira.

Alisema katika mafunzo hayo vijana watajifunza namna bora ya ujenzi kwa kutumia matofali imara yaliyotengenezwa kwa mashine za kisasa za umeme, na kwamba itaboresha elimu yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Veta, Zebadia Moshi, alisema chuo kimefurahishwa na hatua hiyo  itawezesha vijana hao kuongeza ujuzi zaidi na kupanua soko la ajira.

Moshi alisema kumekuwa na tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza chuo hicho kwani asilimia 66 ndiyo hupata ajira, lakini kuanzishwa kwa programu hiyo kutasaidia kusukuma soko la ajira kwa vijana wengi zaidi wanaohitimu mafunzo chuoni hapo

No comments:

Post a Comment