Tuesday, April 16, 2013

SEHEMU YA JENGO LA NHC LAUNGUA,,

Saa chache zilizopita ulizuka moto katika jengo la nyumba ya NHC, lililoko usoni na Al Maksoor karibu na mzunguko (round about) wa Mnara wa Saa (Clock Tower) kwenye barabara ya Uhuru.

Kwa mujibuwa kikosi cha uokozi cha Jeshi la Polisi (kama inavyoonekana kwenye tweets za
WaljiAli zilizopachikwa hapo chini), moto huo kwa sasa tayari umedhibitiwa ingawaje umeunguza nyumba nzima na mali. Hakuna ripoti ya kujeruhiwa ama kufariki kwa mtu yeyote. Chanzo cha kuzuka kwa moto huo bado hakijafahamika bayana.

Shukurani kwa taarifa na picha: Walji Ali (via Twitter)
Picture
Picture
Picture
Picture
Picture

No comments:

Post a Comment