Friday, April 19, 2013

POWERWINDOW ZA MAGARI NUSURA IMUWAHISHE KWA SHETANI










Tukio hilo limetokea mida ya  usiku mara baada ya kijana huyo kukamatwa na vijana wa 4C NINJAS waliokuwa wakifanya ulinzi kwenye magari yaliopaki bara bara  ya migombani( migombani  street) katika eneo la Mikochen na ndipo aliponaswa na kuanza kuambulia kipigo .

awali kijana huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika kutokana na vurugu za kumpiga kuendelea katika eneo hilo ambalo magari yamepaki nje ya bara bara huku wamiliki wake wakiwa kwenye  msiba ,alijitetea kuwa ametoka kazini ambapo  kazini kwake amesema ni karibu na sehemu wanayopaki mabasi ya Summri .


wamiliki hao walionekana kuwa na hasira dhidi ya mtuhumiwa huyo ambaye aliweza kukabiliwa vikali na kuwekwa chini ya ulinzi ili kusubiri maamuzi zaidi hadi Mitambo yetu inaondoka eneo la tukio hatma ya kijana huyo bado haijajulikana mikononi mwa raia hao ambao wamegoma kumpeleka polisi.

No comments:

Post a Comment