Friday, April 12, 2013

MNYIKA AGAWA VITABU NA COMPUTER KATIKA SHULE YA MSINGI MIANZINI ILIYOPO JIMBONI KWAKE

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mianzini iliyopo katika Jimbo la Ubungo Jijini Dar es Salaam, Bw, Swai Elias kushoto akimuelekeza jambo Mbunge wa Ubungo Mhe, John Mnyika leo alipokwenda kutoa vitabu 43 vya Darasa la 1,2, na 5 katika Shule hiyo ikiwa ni namna ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi walioelewa katika Jimbo lake.

Mbunge wa Ubungo John Mnyika akiwagawia wanafunzi wa Darasa la 5 vitabu, vya kingereza ambapo amewataka wazazi kuwa na moyo wa kuwasaidia watoto kwa kuwanunulia vitabu na amewaagiza pia kwa wazazi au mtu yeyote mwenye kitabu cha Kiada au Ziada  akitoe ili wanafunzi wasome bila kujali vitabu hivyo vimetumika na vimechakaa kwa namna gani. Ambapo amesema kuwa kwa wale watakaotaka kuleta vitabu vilivyotumika  wafikishe katika Ofisi ya Mbunge iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mnyika akimkabidhi Mwalimu Mkuu vitabu ambapo ameahidi pia kuiletea shule hiyo Computer Moja kwa ajili ya kufundishia Somo la Tehama kwa Vitendo.

1 comment:

  1. Safi sana.Ni changamoto kwa wazazi,walezi na wadau wote wa elimu kujitoa kwa hali na mali katika kuhakikisha gurudumu la elimu linasonga mbele.Naungana na Mbunge wa Ubungo,ndugu J.Mnyika katika harakati zake za 'TOA KITABU KISOMWE'.

    ReplyDelete